KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema kwamba mshambuliaji Mario Balotelli haendani na mfumo wa sasa wa uchezaji ya Wekundu hao wa Anfield.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao mawili tu tangu ajiunge na timu hiyo kutoka AC Milan kwa dau la Pauni Milioni 16 Agosti mwaka huu na uamuzi wa sasa wa Rodgers unauweka shakani mustakabali wa Mtaliano huyo.
Maisha yake ya Liverpool hayajatawaliwa na migogoro mingi hadi sasa, zaidi ya kufungiwa mechi moja na Chama cha Soka kwa kuposti mambo yaliyotafsiriwa kama udhalilishaji kwenye mitandao ya kijamii.
Mario Balotelli ameshindwa kung'ara Liverpool tangu atue kutoka AC Milan
Kuelekea mechi na Burnley kesho, Rodgers amesema: "Nafikiri tumeona kwamba huo siyo mchezaji wake haswa (mfumo wa 3-4-3).
"Nikiwa nimekwishafanya kazi na Mario aiwa hapa, tumeona kwamba mchezaji huyo ni mzuri anapocheza kwenye boksi, hivyo tunaoutumia kwa sasa hauwezi. Lakini unajaribu kufanya vizuei kutokana na wachezaji ulionao, na ubora ambao unao, hivyo hilo ndilo jambo tunalolifanyia kazi,"amesema.
Brendan Rodgers amesema Balotelli haiendani na mfumo wa uchezaji wa Liverpool
0 comments:
Post a Comment