MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Mario balotelli anakabiliwa na hatari ya kufungiwa mechi na FA baada ya kuposti ujumbe wa kibaguzi kwenye akaunti yake ya Instagram.
Mshambuliaji huyo wa Italia aliposti picha katika akaunti yake ya Instagram ya mchezo wa game wa Super Mario inayosomeka: 'Usiwe mbaguzi — kuwa kama Mario. Ni fundi wa Kitaliano aliyetengenezwa na watu wa Japan wanaozungumza Kiingereza na kuonekana kama wa Wamexico,”.
Na chini ya picha hiyo kulikuwa kuna maneno yasemayo: '... Ruka kama mtu mweusi na kamata sarafu kama Mnahudi,”.'
Balotelli mwenye umri wa miaka 24, akijibu shutuma dhidi yake kutokana na ujumbe wake mtandaoni aliandika tena ujumbe usemao; “Mama yangu ni Myahudi, wote nyamazeni kimya”.
Hata hivyo, Balotelli anadaiwa kuufuta haraka haraka ujumbe wa awali aliouandika ambao unadaiwa kuwa ni wakibaguzi. Msemaji wa Liverpool, amekiri kuwa na taarifa ya ujumbe huo na kwamba watafanya mazungumzo na Balotelli.
FA ya England imesema ina taarifa za mchezaji huyo kuiweka taarifa hiyo katika Instagram kabla ya kuifuta baadaye kidogo.
Nyota wa Liverpool, Mario Balotelli ameposti picha jana ambayo inaweza kumsababishia matatizo
0 comments:
Post a Comment