KLABU ya Azam FC imemsajili winga wa kimataifa wa Uganda, Brian Majwega leo mjini Kampala, Uganda.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema kwamba, winga huyo wa KCCA ya Kampala, Uganda amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na mabingwa hao wa Tanzania Bara.
Kawemba amesema kwamba Majwega anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Azam FC katika dirisha dogo baada ya beki Serge Wawa Pascal kutoka Ivory Coast, aliyekuwa anacheza El Merreikh ya Sudan na Amri Kiemba aliyekuwa Simba SC, ambaye amesainiwa kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.
Majwega amesaini leo mjini Kampala na moja kwa moja kujiunga na kikosi cha timu hiyo, chini ya makocha Mcameroon Joseph Marius Omog na Mganda George ‘Best’ Nsimbe ambacho kipo kambini mjini humo tangu juzi hadi Desemba 22, mwaka huu.

Brian Majwega akiwa na jezi ya Azam FC baada ya kusaini leo mjini Kampala, Uganda |
Menaja wa Azam FC, Jemadari Said kulia akimkabidhi jezi Majwega leo Kampala baada ya kusaini Mkataba wa miaka miwili |
Majwega amesaini leo mjini Kampala na moja kwa moja kujiunga na kikosi cha timu hiyo, chini ya makocha Mcameroon Joseph Marius Omog na Mganda George ‘Best’ Nsimbe ambacho kipo kambini mjini humo tangu juzi hadi Desemba 22, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment