ARSENAL imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham United ugenini katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku huu.
Nahodha wa West Ham, Alex Song aliifunga timu yake ya zamani baada ya shuti lake zuri la umbali wa mita 25 kutinga nyavuni, lakini mshika kibendera namba moja akaseka alikuwa ameotea.
Santi Cazorla akafunga kwa penalti dakika ya 41 na Danny Welbeck akafunga la pili dakika ya 44 kuifanya Arsenal iomgoze kwa mabao 2-0 hadi mapumziko.
Cheikhou Kouyate akaifungia bao la kufutia machozi West Ham dakika ya 54 kwa kichwa akimalizia krosi ya James Tomkins.
Kikosi cha West Ham kilikuwa; Adrian, O’Brien/Demel dk78, Reid, Tomkins, Cresswell, Kouyate/Nolan dk78, Song, Amalfitano, Downing, Carroll na Sakho/Valencia dk62.
Arsenal; Szczesny, Debuchy, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Coquelin, Flamini, Oxlade-Chamberlain/Chambers dk90, Cazorla, Welbeck/Gibbs dk84 na Sanchez.
Mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez (katikati) akipambana na Alex Song wa West Ham
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2889186/West-Ham-1-2-Arsenal-Santi-Cazorla-Danny-Welbeck-strike-quick-succession-Gunners-bump-Hammers-fifth.html#ixzz3NDUYrsoF
0 comments:
Post a Comment