// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ARSENAL YAICHAPA NEWCASTLE 4-1 EMIRATES - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ARSENAL YAICHAPA NEWCASTLE 4-1 EMIRATES - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, December 13, 2014

    ARSENAL YAICHAPA NEWCASTLE 4-1 EMIRATES

    ARSENAL imeichapa mabao 4-1 Newcastle katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Emirates, London. 
    The Gunners walianza na moto na Nahodha Per Mertesacker almanusra afunge bao la mapema baada ya kupiga kichwa kilichogonga mwamba wa juu.
    Olivier Giroud akaifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya 15, kabla ya Danny Welbeck kufunga bao lililokataliwa kwa kudaiwa alimchezwa rafu Daryl Janmaat wa Newcastle.
    Santi Cazorla akaifungia The Gunners bao la pili dakika ya 54, kabla ya Giroud kufunga tena dakika ya 58 akimalizia krosi ya Hector Bellerin.
    Santi Cazorla scored twice as Arsenal defeated Newcastle 4-1 in the Premier League on Saturday evening
    Santi Cazorla akishangilia baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 

    Ayoze Perez akaifungia bao la kufutia machozi The Magpies kwa kichwa dakika ya 60, kabla ya Cazorla kuhitimisha ushindi wa Arsenal kwa bao la nne dakika ya 88 kwa penalti baada ya Welbeck kuchezewa rafu.
    Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Bellerin, Debuchy, Mertesacker, Gibbs, Flamini, Sanchez/Coquelin dk87, Oxlade-Chamberlain/Maitland-Niles dk90, Cazorla, Welbeck na Giroud/Podolski dk73.

    Newcastle: Alnwick, Janmaat, Coloccini, Williamson, Dummett, Tiote, Colback, Gouffran, Perez/Armstrong dk82, Ameobi/Riviere dk56 na Cisse/Cabella dk56.Welbeck (right) was brought down inside the Newcastle penalty area by left back Paul Dummett in the dying moments of the match
    Danny Welbeck (kulia) akiangushwa chini na beki wa kushoto wa Newcastle, Paul Dummett na kusababisha penalti

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2872819/Arsenal-4-1-Newcastle-Olivier-Giroud-Santi-Cazorla-score-twice-Arsene-Wenger-s-produce-impressive-performance.html#ixzz3LoTgJj6T 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA NEWCASTLE 4-1 EMIRATES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top