BONDIA Muingereza mwenye asili ya India, Amir Khan amemshinda kwa pointi mpinzani wake Devon Alexander katika pambano la raundi 10 uzito wa Welter Alfajiri ya leo ukumbi wa MGM Grand, las Vegas, Marekani.
Khan alimzidi mno mpinzani wake huyo na kutawala raundi zote na kwa kiwango hicho amejitengenezea mazingira ya kuzipiga na Floyd Mayweather mwakani.
Khan alirusha jumla ya ngumi 563 dhidi ya 461 za mpinzani wake, huku 243 zikimfika vyema Devon aliyefanikiwa kufikisha makonde 91 pia kwa Muhindi huyo.
Wengi wanaamini Khan atakuwa mpinzani sahihi ajaye wa Mayweather kufuatia kumpiga bingwa wa dunia mara tatu, Devon. Mayweather amekwishasema atapigana na Manny Pacquiao Mei 1 mwakani, lakini kuna uwezekano akaanza Khan.
Amir Khan akimtupia konde Alexander (kushoto) na kulia akishangilia na promota Oscar de la Hoya (kulia)
Khan akimuadhibu Alexander
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/boxing/article-2873119/Amir-Khan-dominates-Devon-Alexander-Las-Vegas-Brit-face-Floyd-Mayweather-Jr.html#ixzz3LrrypmNU
0 comments:
Post a Comment