MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Shirikisho la Mashabiki jana.
Mpachika mabao huyo wa mabingwa wa Ligi Kuu ya England na washindi wa pili wa Kombe la Dunia, Argentina, alishinda tuzo hiyo katika hoteli ya St Pancras Renaissance mjini London, England.
Sergio Aguero akiwa na tuzo yake kwa pamoja na mpenzi wake, Karina Tejeda
Nahodha wa Manchester United na England, Wayne Rooney na winga wa Real Madrid na Wales, Gareth Bale pia walikuwemo kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hiyo sambamba na nyota wengine wa Ligi Kuu England, Thibaut Courtois, Branislav Ivanovic, Vincent Kompany, Pablo Zabaleta, Angel di Maria, Cesc Fabregas, Eden Hazard, Mesut Ozil, Yaya Toure, Sergio Aguero na Diego Costa.
0 comments:
Post a Comment