KAKA wa Emmanuel Adebayor, Kola amesema kwamba mshambuliaji huyo amevurgwa na imani na kiislamu kiasi cha kufikiria mama yao anawaloga ili asing'are uwanjani.
Kola, mwenye umri wa miaka 42, dereva wa lori mjini Bremen, Ujerumani, ameiambia The Sun jana kwamba: "[Emmanuel] amevurugwa na Waislamu wanaomuambia sababu za kufunga mabao na kwa nini hafanyi vizuri kwa sasa akicheza.
"Wanamshawishi kwamba dada yake na mama yake wanamloga. Mama yangu ana machungu sana. Kila siku analia. Nimezungumza naye kwenye simu na alilia tena,".amesema.
Kaka yake Emmanuel Adebayor, Kola amekasirishwa na kitendo cha mdogo wake kumnyanyasa mama yaoe, Alice
Hivi karibuni Adebayor alikanusha madai ya dada yake, Maggie kwamba alimfukuza mama yao, Alice katika nyumba yao Afrika kwa sababu anafikiri anamloga.
Dada huyo huyo wa Ade Mabao aisema kwamba mama yao alikuwa anauza mifuko ya nailoni na kufuli na vitu vingine kuilea familia yake, pamoja na hayo Emmanuel akasema mama yao aliondoka nyumbani kwa sababu zake.
Adebayor, akizungumza na kituo cha Redio cha Peace FM, amesema: "Sikuwahi kumfukuza mama yangu nyumbani. Aliamua kuondoka mwenyewe. Nitawezaje kuguswa na mama yangu ambaye anamuambia kila mmoja kazi yangu haitasionga mbele, hivyo lazima nitakuwa upande wangu na kufanya yangu,"amesema.
0 comments:
Post a Comment