MABINGWA watetezi, Manchester City wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Swansea City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Etihad.
Wilfried Bony alitangulia kuifungia Swansea mapema dakika ya tisa akimalizia pasi ya Nathan Dyer kabla ya Stevan Jovetic kuisawazishia City dakika 10 baadaye.
Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure ndiye aliyeihakikishia Man City inayofundishwa na Manuel Pellegrini pointi tatu kwa bao lake dakika ya 62.
Kikosi cha Manchester City kilikuwa; Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Fernandinho/Fernando dk88, Toure, Navas, Nasri/Milner dk79, Jovetic/Lampard dk70 na Aguero.
Swansea City: Fabianski, Rangel, Bartley, Williams, Taylor, Ki, Carroll/Shelvey dk67, Sigurdsson/Gomis dk79, Dyer/Barrow dk77, Montero na Bony.
Yaya Toure proved Manchester City's matchwinner as they defeated Swansea 2-1 in the Premier League
Toure (centre) scored City's winner midway through the second half after bursting into the penalty box before firing home a late shot
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2845404/Manchester-City-2-1-Swansea-Stevan-Jovetic-Yaya-Toure-goals-cancel-Wilfried-Bony-s-opener-hosts-win.html#ixzz3JovBpz1Z
0 comments:
Post a Comment