GWIJI wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry anaweza kurejea katika klabu hiyo kwa mara ya tatu, lakini safari hii kama kocha si mchezaji tena, amesema Arsene Wenge.
Henry’ anamaliza Mkataba wake katika klabu ya New York Red Bulls mwezi ujao mwishoni mwa msimu wa Ligi Kuu ya Marekani, MLS na ingawa hajatangaza kama atastaafu, lakini wengi wanaamini utakuwa mwisho wake wa kucheza.
"Siyo haiwezekani," amesema Wenger, alipoulizwa kama mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37- Nahodha wa zamani wa Arsenal atarejea kukochi. "Nawakaribisha watu walituchezea kurudi (kwa sababu) ya kazi ya heshima,".
Henry (kushoto) akisherehekea na moja ya mataji mawili ya Ligi alishinda akiwa na Robert Pires (katikati) na Sol Campbell (kulia)
Wenger anaamini Henry ana ubora wa kuwa kocha
‘Itakuwa kazi ambayo ipo na ambayo unadamka asubuhi na kufanya kitu fulani,"amesema.
Henry amewahi kusema angependa kuifundisha Arsenal, wakati anachezea klabu hiyo katika miaka yake minane, ambayo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu na kuwa mfungaji bora wa kihistoria wa klabu kabla ya kutimkia Barcelona mwaka 2007.
Alirejea kwa muda kwa mkopo kutoka New York Januari mwaka 2012 na alifunga jumla ya mabao 228 katika klabu hiyo ya Kaskazini mwa London. Wenger amesema: "Ana ubora wa kuwa kocha? Ndiyo... lakini anatakiwa kuamua kujitoa mhanga maisha yake. Wakati unapokuwa mchezaji, unafikiri ni rahisi mho kuwa kocha. Unapokuwa kocha, unafikiri ni mkanganyiko mno na kama hujajiandaa kwa hilo huwezi kudumu.
"Ubora mmoja ambao unatakiwa kuwa nao ni kuweza kumudu kukandiwa, unapohisi haiko sawa. Sijui ni vipi atamudu hiyo," amesema.
0 comments:
Post a Comment