// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WELBECK AIPA POINTI TATU ARSENAL LIGI KUU ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WELBECK AIPA POINTI TATU ARSENAL LIGI KUU ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, November 29, 2014

    WELBECK AIPA POINTI TATU ARSENAL LIGI KUU ENGLAND

    BAO pekee la mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Danny Welbeck limeipa Arsenal ushindi wa 1-0 dhidi ya West Bromwich Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni hii Uwanja wa The Hawthorns.
    Danny alifunga bao hilo kwa kichwa dakika ya 59 akimalizia mpira uliopigwa na Santi Cazorla na sasa The Gunners inasogea nafasi ya nne kabla ya matokeo ya mechi nyingine za wikiendi hii.
    Saido Berahino aligongesha mwamba dakika 10 za mwishoni katika harakati za kusaka bao la kusawazisha na sasa West Brom inafikisha mechi saba bila kushinda Hawthorns msimu huu, jambo ambalo lilifanya wazomewe na mashabiki wao mwishoni mwa mchezo.
    Kikosi cha West Brom kilikuwa: Foster, Wisdom, Dawson, Lescott, Pocognoli/Gamboa dk74, Mulumbu/Anichebe dk65, Gardner, Dorrans, Sessegnon/Samaras dk76, Brunt na Berahino.
    Arsenal: Martinez, Chambers, Mertesacker, Koscielny Monreal/Gibbs dk23, Ramsey, Flamini, Sanchez, Cazorla, Welbeck na Giroud/Oxlade-Chamberlain dk78. 
    The England international rose highest to head the Gunners in front after Ben Foster failed to keep out his attempt
    Danny Welbeck akiwa hewani kupiga kichwa kuifungia The Gunners huku kipa Ben Foster akishindwa kuunasa mpita
    Welbeck runs away in celebration following his sixth Arsenal goal of the season, which turned out to be the winner at the Emirates
    Welbeck akikimbia kushangilia baada ya kuifungia bao la ushindi Arsenal 

    PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2854068/West-Brom-0-1-Arsenal-Danny-Welbeck-fires-Gunners-crucial-victory-Hawthorns.html#ixzz3KTCDHwIR 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WELBECK AIPA POINTI TATU ARSENAL LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top