// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WATANZANIA KUPIGIA KURA JEZI YA TIMU YA TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WATANZANIA KUPIGIA KURA JEZI YA TIMU YA TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, November 25, 2014

    WATANZANIA KUPIGIA KURA JEZI YA TIMU YA TAIFA

    "Watanzania wanatakiwa kupigia kura jezi ya timu ya Taifa ya nyumbani na ugenini kupitia mtandao wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa www.tff.or.tz ambapo jezi hizo zimewekwa.
    TFF ilipokea mapendekezo ya mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa kutoka kwa Watanzania 86. Jezi 11 za nyumbani, bukta nane za nyumbani, jezi nane za ugenini na bukta tano za ugenini ndizo zimepitishwa kwa ajili ya kupigiwa kura.
    Mwisho wa kupiga kura ni Desemba 31 mwaka huu. Mpigaji kura anatakiwa kubonyeza kwenye jezi na bukta ambayo ameichagua. Anatakiwa kufanya hivyo kwa jezi ya nyumbani na jezi ya ugenini.
    Tunawashukuru wote waliojitokeza kupendekeza mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa,". IMETOLEWA NA TFF.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WATANZANIA KUPIGIA KURA JEZI YA TIMU YA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top