// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WATANO WAUNDA JOPO KUHAKIKI UMRI COPA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WATANO WAUNDA JOPO KUHAKIKI UMRI COPA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Wednesday, November 12, 2014

        WATANO WAUNDA JOPO KUHAKIKI UMRI COPA

        Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
        KAMATI ya Vijana ya Shirikisho la SOKA Tanzania (TFF) imeunda jopo la watu watano kuhakiki umri wa wachezaji watakaoshiriki hatua ya ngazi ya Taifa ya michuano ya Copa Coca-Cola 2014.
        Michuano hiyo ya ngazi ya Taifa itafanyika Dar es Salaam kuanzia Desemba 13 hadi 20 mwaka huu. Uhakiki wa umri utafanyika Desemba 11 na 12 mwaka huu wakati timu zote zinatakiwa kuwasili Shule ya Filbert Bayi mkoani Pwani kuanzia Desemba 10 mwaka huu.
        Jopo hilo la uhakiki linaongozwa na Mkufunzi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Henry Tandau. Wengine katika jopo hilo ni Ally Mayay, Charles Boniface Mkwasa, Dk. Jonas Tiboroha na Richard Yomba.
        Charles Boniface Mkwasa yumo

        Timu 16 zitakazocheza michuano hiyo inayoshirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15 ni Arusha, Dodoma, Geita, Katavi, Kigoma, Kinondoni, Kusini Pemba, Kusini Unguja, Lindi, Mbeya, Mjini Magharibi, Morogoro, Mwanza, Ruvuma, Simiyu na Tanga.
        Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa vinakumbushwa kutuma TFF fomu za usajili ambazo zinatakiwa kuambatanishwa vyeti vya kuzaliwa vya wachezaji husika.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: WATANO WAUNDA JOPO KUHAKIKI UMRI COPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry