// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); UGANDA YASHINDWA KUTIMIZA NDOTO ZA KUFUZU AFCON, IKICHEZA PUNGUFU NA KUPIGWA 2-0 NA GUINEA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE UGANDA YASHINDWA KUTIMIZA NDOTO ZA KUFUZU AFCON, IKICHEZA PUNGUFU NA KUPIGWA 2-0 NA GUINEA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, November 19, 2014

    UGANDA YASHINDWA KUTIMIZA NDOTO ZA KUFUZU AFCON, IKICHEZA PUNGUFU NA KUPIGWA 2-0 NA GUINEA

    UGANDA imeshindwa kutimiza ndoto za kucheza tena Fainali za Mataifa ya Afrika tangu ilipocheza mara ya mwisho mwaka 1978, kufuatia kuzidiwa kete na Guinea leo.
    Ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja, baada ya Nahodha Andy Mwesigwa kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kucheza rafu, Uganda imechapwa mabao 2-0 na wenyeji Guinea katika mchezo wa Kundi E kufuzu AFCON.

    Mabao ya Guinea yamefungwa na Ibrahima Traore dakika ya 29 na Seydouba Soumah dakika ya 61 kwa penalti baada ya rafu ya Mwesigwa kwenye boksi dakika ya 59.
    Guinea inafikisha pointi 10 na kuungana na Ghana iliyoongoza Kundi kwa pointi zake 11 kwenda Equatorial Guinea kwenye fainali za AFCON mapema mwakani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UGANDA YASHINDWA KUTIMIZA NDOTO ZA KUFUZU AFCON, IKICHEZA PUNGUFU NA KUPIGWA 2-0 NA GUINEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top