// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); UGANDA WAHITAJI HATA SARE UGENINI KESHO KUFUZU AFCON, MICHO AOMBA DUA ZA WATANZANIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE UGANDA WAHITAJI HATA SARE UGENINI KESHO KUFUZU AFCON, MICHO AOMBA DUA ZA WATANZANIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, November 18, 2014

    UGANDA WAHITAJI HATA SARE UGENINI KESHO KUFUZU AFCON, MICHO AOMBA DUA ZA WATANZANIA

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    UGANDA inahitaji ushindi wa ugenini kesho kujikatia tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 36 na kocha Mserbia Milutin Sredojevic ‘Micho’ ameomba duwa za raia wote wa Afrika Mashariki atimize dhamira.
    The Cranes watakuwa wageni wa Guinea mjini Conakry kuanzia Saa 1:00 usiku kesho na japokuwa inaweza ikafuzu hata ikipata sare, iwapo 
    Ghana itaifunga Togo mjini Accra, lakini ushindi ndio kila kitu.
    Ghana wanaongoza Kundi E kwa pointi zao nane na kesho watacheza Togo nyumbani, wakihitaji lazima ushindi ili kujihakikishia kwenda Equatorial Guinea Januari mwakani.
    Kocha wa Uganda, Micho kushoto ameomba dua za Watanzania afuzu AFCON kesho 

    GONGA HAPA KUANGALIA RATIBA KAMILI MECHI ZA MWISHO KUFUZU AFCON http://www.supersport.com/football/africa-cup-of-nations/fixtures
    MISIMAMO YA MAKUNDI YOTE
    http://www.supersport.com/football/africa-cup-of-nations/logs
    Kila la heri ndugu zetu Uganda, Mungu awabariki mfanikiwe kufuzu AFCON
    Hiyo inatokana na kwamba, Togo yenye pointi sita ikishinda itafikisha tisa na kuweza kuungana na ama Uganda au Guinea zenye pointi saba kwa sasa kwenda AFCON ya mwakani.
    “Natumaini nitakuwa kwenye dua na sala za ndugu zangu wote wa Tanzania Jumatano, kama ambavyo natarajia kwa watu wengine wote wa Afrika Mashariki hususan watu wa mpira,”amesema Micho leo akizungumza kwa simu na BIN ZUBEIRY. 
    Mara ya mwisho Uganda kucheza AFCON, ilikuwa mwaka 1978 wakati huo bado inaitwa michuano ya Kombe la Mataifa Huru Afrika, walipofanikiwa kufika Fainali na kufungwa 2-0 na Ghana Uwanja wa Accra Sports mjini Accra, mabao ya Opoku Afriyie ‘Bayie’ dakika ya 38 na 64.
    Kwa ujumla Uganda imecheza fainali nne za AFCON, 1962 iliposhika nafasi ya nne, 1968 walipotolewa Raundi ya Kwanza, sawa na 1974 na 1976, kabla ya hiyo ya kufika Fainali 1978.
    Mserbia huyo amesema anashukuru kikosi chake au wachezaji wake wote wako vizuri kuelekea mchezo huo na wameonyesha dhamira ya kushinda ili kuitoa kimasomaso nchi yao.
    Mechi za mwisho za kufuzu AFCON zinafanyika leo na jumla ya nyasi za viwanja 15 zitawaka moto kuanzia jioni hadi usiku.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UGANDA WAHITAJI HATA SARE UGENINI KESHO KUFUZU AFCON, MICHO AOMBA DUA ZA WATANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top