Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MIKOA ya Simiyu na Kigoma itakutana uso kwa uso kwenye mechi ya fungua dimba la fainali za Taifa za mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 15 ya Copa Coca-Cola itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam Desemba 13.
Timu za wavulana zimegawanywa katika makundi manne wakati timu za wasichana zimegawanywa katika makundi mawili na fainali hizo zimepangwa kufikia tamati Desemba 20, mwaka huu.
Kundi A kwa timu za wavulana linajumuisha timu za Simiyu, Mbeya, Lindi na Kigoma wakati Kundi B limeundwa na timu za Katavi, Dodoma, Ruvuma na Mjini Magharibi. Kundi C lina timu za Kinondoni, Arusha, Mwanza na Geita wakati Kundi D linaundwa na Kusini Pemba, Kusini Unguja, Morogoro na Tanga.
Mikoa hiyo imefika hatua ya 16 bora baada ya kushinda katika hatua ya mkoa ambako timu 32 zilishiriki kwa mtindo wa mechi mbili za nyumbani na ugenini.
Timu za wasichana kutoka mikoa ya Temeke, Mwanza, Mbeya, Kinondoni, Zanzibar, Dodoma, Ilala na Arusha hazikuwa na mchujo katika hatua ya mkoa hivyo kuingia moja kwa moja kwenye fainali za taifa.

0 comments:
Post a Comment