// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SAMATTA NJE TUZO ZA WANASOKA BORA AFRIKA, YAYA TOURE AINGIA KUTETEA TAJI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SAMATTA NJE TUZO ZA WANASOKA BORA AFRIKA, YAYA TOURE AINGIA KUTETEA TAJI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, November 08, 2014

    SAMATTA NJE TUZO ZA WANASOKA BORA AFRIKA, YAYA TOURE AINGIA KUTETEA TAJI

    SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya wachezaji wa kuwnaai tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika  na Mwanasoka Bora Nayecheza Afrika mwaka 2014.
    Yaya Toure wa Ivory Coast anayeshikilia tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika amerudi kutetea tuzo yake, akipambanishwa na wakali kama Emanuel Adebayor wa Togo, Ahmed Musa wa Nigeria na Kwado Asamoah wa Ghana.
    Mtanzania Mbwana Samatta pamoja na kuendelea kufanya vizuri akiwa na TP Mazembe ya DRC, lakini hajaingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo ya Wachezaji wanaocheza Afrika.
    Yaya Toure amefanikiwa kuingia kutetea tuzo yake
    Wachezaji 25 wameingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika, wakati wengine 20 watawania tuzo ya Mchezaji anayecheza Afrika.
    Washindi wa vipengele hivyo viwili watapatikana baada ya kura zitakazopigwa na Makocha Wakuu na Wakurugenzi wa Ufundi wa vyama vya soka na Mashirikisho wanachama wa CAF.
    Sherehe za tuzo zitafanyika Alhamisi ya Januari 8, mwakani mjini Lagos, Nigeria. Wakati Yaya Toure anashikilia tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika, Mohamed Aboutreika wa Misri anashikilia tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika na kwa bahati mbaya hajaingia kutetea tuzo yake. 
    WANAOWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA
    1.    Ahmed Musa             (Nigeria, CSKA Moscow)
    2.    Asamoah Gyan         (Ghana, Al Ain)
    3.    Dame N’doye           (Senegal, Lokomotiv Moscow)
    4.    Emmanuel Adebayor (Togo, Tottenham)
    5.    Eric Maxim Choupo-Moting   (Cameroon, Schalke 04)
    6.    Fakhreddine Ben Youssef     (Tunisia, CS Sfaxien)
    7.    Ferdjani Sassi                   (Tunisia, CS Sfaxien)
    8.    Yao Kouassi Gervais ‘Gervinho’ (Ivory Coast, AS Roma)
    9.    Islam Slimani             (Algeria, Sporting Lisbon) 
    10. Kwadwo Asamoah     (Ghana, Juventus)
    11. Mehdi Benatia           (Morocco, Bayern Munich)
    12. Mohamed El Neny     (Misri, Basel)
    13. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon, Borussia Dortmund) 
    14. Raïs M'Bolhi             (Algeria, Philadelphia Union) 
    15. Sadio Mané               (Senegal, Southampton)
    16. Seydou Kieta             (Mali, As Roma)
    17. Sofiane Feghouli       (Algeria, Valencia)
    18. Stephane Mbia         (Cameroon,  Sevilla)
    19. Thulani Serero           (Afrika Kusini, Ajax)
    20. Vincent Aboubakar     (Cameroon, Porto) 
    21. Vincent Enyeama       (Nigeria, Lille)
    22. Wilfried Bony             (Ivory Coast, Swansea)
    23. Yacine Brahimi         (Algeria, Porto)
    24. Yannick Bolasie         (DRC, Crystal Palace)
    25. Yaya Toure               (Ivory Coast, Man City)
    Mbwana Samatta hajaingia kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora anayecheza Afrika licha ya kuendelea kufanya vizuri TP Mazembe 

    WANAOWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA ANAYECHEZA AFRIKA
    1.    Amr Gamal               (Misri, Al Ahly)
    2.    Abdelrahman Fetori   (Libya, Ahly Benghazi)
    3.    Bernard Parker         (Afrika Kusini, Kaizer Chiefs)
    4.    Bongani Ndulula         (Afrika Kusini, Amazulu)
    5.    Akram Djahnit           (Algeria, ES Setif)
    6.    Ejike Uzoenyi             (Nigeria, Enugu Rangers)
    7.    El Hedi Belamieri       (Algeria, ES Setif)
    8.    Fakhereddine Ben Youssef   (Tunisia, CS Sfaxien)
    9.    Ferdjani Sassi                    (Tunisia, CS Sfaxien)
    10. Firmin Mubel Ndombe          (DRC, AS Vita)
    11. Geoffrey Massa                  (Uganda, Pretoria University)
    12. Jean Kasusula                     (DRC, TP Mazembe)
    13. Kader Bidimbou                  (Kongo, AC Leopards)
    14. Lema Mabidi                       (DRC, As Vita)
    15. Mudathir Al Taieb                (Sudan, Al Hilal)
    16. Roger Assalé                     (Ivory Coast, Sewe Sport)
    17. Senzo Meyiwa                    (Afrika Kusini, Orlando Pirates)
    18. Solomon Asante                 (Ghana, TP Mazembe)
    19. Souleymane Moussa            (Cameroon, Coton Sport)
    20. Yunus Sentamu                  (Uganda, AS Vita)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA NJE TUZO ZA WANASOKA BORA AFRIKA, YAYA TOURE AINGIA KUTETEA TAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top