// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SAAD KAWEMBA ‘ALIYENG’ARA’ TFF YA TENGA AWA MTENDAJI MKUU AZAM FC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SAAD KAWEMBA ‘ALIYENG’ARA’ TFF YA TENGA AWA MTENDAJI MKUU AZAM FC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, November 25, 2014

    SAAD KAWEMBA ‘ALIYENG’ARA’ TFF YA TENGA AWA MTENDAJI MKUU AZAM FC

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Saad Kawemba ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam.
    Kawemba ametambulishwa rasmi leo na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Sheikh Said Muhammad makao makuu ya klabu, Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    “Nafurahi kupata nafasi hii, ni fursa nyingine tena ya kupata uzoefu mwingine katika uongozi wa soka baada ya kufanya kazi kwa mafanikio TFF,”amesema Kawemba.
    Saad Kawemba kushoto amekuwa Mtendaji Mkuu wa Azam FC

    Bodi ya Ukurugenzi ya Azam FC imefikia hatua ya kuajiri Mtendaji Mkuu, ili kurahisisha uendeshaji ndani ya klabu kwa lengo la kutafuta ufanisi zaidi.
    Kawemba ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba anatarajia kupata ushirikiano mzuri kutoka kwa Bodi, Menejimenti na wafanyakazi wote wa klabu hiyo bingwa Tanzania Bara.
    Kawemba alifanya kazi TFF wakati wa Rais, Leodegar Chilla Tenga kabla ya kuondolewa baada ya kuingia uongozi mpya, chini ya Rais, Jamal Malinzi Oktoba mwaka jana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAAD KAWEMBA ‘ALIYENG’ARA’ TFF YA TENGA AWA MTENDAJI MKUU AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top