BAO pekee la Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo limeipa ushindi wa 1-0 ugenini Real Madrid dhidi ya FC Basle katika mchezo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu.
Mreno huyo, aliyeondoka Manchester United kutua Madrid kwa dau la rekodi, alifunga bao hilo pekee muhimu dakika ya 35 akimalizia kazi nzuri ya Mfaranda, Karim Benzema.
Real Madrid sasa inaongoza Kundi B kwa rekodi nzuri ya ushindi, huku ikiwa imesaliwa na mecni moja, wakati kwa kipigo cha leo, Basle hatima yao itajulikana baada ya mechi ya mwisho dhidi ya Liverpool kama watasonga mbele au, la.
Kikosi cha Basle kilikuwa; Vaclik, Degen/Hamoudi dk76, Schar, Suchy, Safari, Elneny, Frei/Diaz dk83, Zuffi/Kakitani dk87, Gonzalez, Embolo na Gashi.
Real Madrid: Navas, Arbeloa, Varane, Ramos, Coentrao, Kroos, Isco/Nacho dk93, Rodriguez/Marcelo dk89, Bale, Ronaldo na Benzema/Illarramendi dk71.
Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Real Madrid
Gareth Bale wa Real Madrid akipambana na beki wa Basle, Philipp Degen
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2850941/Basle-0-1-Real-Madrid-Cristiano-Ronaldo-bundles-home-Lionel-Messi-toes.html#ixzz3KDcQmJLf
0 comments:
Post a Comment