WINGA Gareth Bale, beki Sergio Ramos na kocha wao, Carlo Ancelotti have been celebrating after winning 16 straight games wamesherehekea kushinda mechi 16 mfululizo kwa mara ya kwanza katika historia ya Real Madrid.
Watatu hao wameposti picha kwenye Twitter jana usiku bada ya kuifunga Malaga 2-1, mabao ya Karim Benzema na Bale na kuweka rekodi, wakishikilia vidole 16 baina yao na Ramos akasema: 'A seguir trabajando. Buenas noches..!! maana yake Acha tuendelee kupiga kazi. Usiku mwema..!!.'
Ushindi huo wa La Liga unaifanya klabu hiyo ipiku rekodi ya mechi 15 iliyowekwa na Miguel Munoz msimu wa 1960-61 na kufikiwa pia na Jose Mourinho msimu wa 2011-12.
Gareth Bale, Carlo Ancelotti na Sergio Ramos wakiwa wameshikilia vidole 16 kushangilia wimbi la ushindi la Real
Bale (kushoto) akishangilia na Karim Benzema usiku wa jana baada ya kuichapa 2-1 Malaga
0 comments:
Post a Comment