// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RANGERS YATOA SARE 1-1 NA AFRICAN SPORTS MKWAKWANI MBIO ZA LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RANGERS YATOA SARE 1-1 NA AFRICAN SPORTS MKWAKWANI MBIO ZA LIGI KUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, November 19, 2014

    RANGERS YATOA SARE 1-1 NA AFRICAN SPORTS MKWAKWANI MBIO ZA LIGI KUU

    FRIENDS Rangers ya Manzese, Dar es Salaam leo imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji African Sports Uwanja Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
    Rangers sasa inafikisha pointi 21 baada ya kucheza mechi 11, ikiendelea kubaki nafasi ya pili nyuma ya Majimaji yenye pointi 21 pia, lakini ina wastani mzuri zaidi wa mabao.
    Hata hivyo, Majimaji ina kiporo cha mechi moja katika Kundi hilo A, ambayo watacheza kesho na Kimondo Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

    Katika mchezo wa leo Uwanja wa Mkwakwani, Rangers ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao, lililofungwa na Idrisa Ismail dakika ya 10, kabla ya Sports kusawazisha kupitia kwa Maulid Abbas dakika ya 85.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RANGERS YATOA SARE 1-1 NA AFRICAN SPORTS MKWAKWANI MBIO ZA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top