Na Vincent Opiyo, NAIROBI
AIDHA Gor Mahia FC au Sofapaka FC atatawazwa bingwa wa ligi kuu kesho Jumamosi ambayo ni siku ya mwisho ya msimu wa elfu mbili na kumi na nne nchini Kenya.
Gor ambaye ni bingwa mtetezi atahitaji ushindi dhidi ya Ushuru FC uwanjani Moi mjini Kisumu ili kuhifadhi taji hilo kwa mara ya pili mfululizo na iwapo atateleza basi Sofapaka huenda wakampokonya taji hilo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009 iwapo tu watamzaba Tusker FC ambaye amepoteza mtanange mmoja tu akiwa nyumbani.
Gor Mahia maarufu kama K’Ogalo wanaongoza jedwali la timu kumi na sita kwa alama 57, alama moja tu zaidi ya nambari mbili Sofapaka ukipenda Batoto ba Mungu huku Tusker FC akiwa wa tatu kwa alama 52 baada ya kusakata mechi 29.
Habari zinazowatia hofu mashabiki wa Gor hata hivyo ni kutokuwepo kwa kiungo raia wa Uganda Geoffrey ‘Baba’ Kizito ambaye atatumikia adhabu ya mechi moja kwa kupokezwa kadi tano za manjano nao vijana wake kocha mganda Sam Timbe Sofapaka wazikose huduma za mabeki Eugine Asike na Collins Shivachi kwa kutunukiwa kadi za manjano kumi na nyekundu mtawalia.
Katika mechi zingine, Bandari atakuwa mwenyeji wa AFC Leopards mjini Mombasa, SoNy Sugar kuandaa zulia la Awendo kumenyana na wanajeshi wa Ulinzi Stars, Thika United na Chemelil Sugar wapepetane katika uwanja wa Kaunti ya Thika, Muhoroni Youth isafiri mjini Kakamega kugaragazana na Western Stima huku vita vya nani atakayeshuka ngazi vikiwa baina ya Nairobi City Stars na Mathare United nao KCB wadanedane na Top Fry AllStars uwanjani City, Nairobi.
Ili kuepuka shoka, City Stars ambao wamo nambari kumi na tano kwenye jedwali watahitaji ushindi wa mabao 8 – 0 dhidi ya Mathare United watakao kuwa bila kiungo Vincent Okello (adhabu ya mechi moja) iwapo tu Top Fry ambaye ameshushwa daraja tayari wamzima nambari kumi na nne KCB. Mechi zote zitang’oa nanga mwendo wa saa nane alasiri.

Gor Mahia watatetea ubingwa wa Kenya kesho? |

0 comments:
Post a Comment