NYOTA wa Barcelona, Neymar amefunga mabao mawili katika ushindi wa 4-0 wa timu yake ya taifa, Brazil dhidi ya Uturuki usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Sukru Saracoglu.
Neymar aliwafungia bao la kwanza mabingwa hao mara tano wa Kombe la Dunia dakika ya 20, kabla ya beki wa Uturuki, Semih Kaya kujifunga kuipatia Brazil bao la pili dakika ya 24.
Willian akawafungia Brazil bao la tatu dakika ya 44, kabla ya Nahodha Neymar kuhitimisha ‘pati la mabao’ kwa kuifunga bao la nne timu ya Carlos Dunga dakika ya 60.
Kikosi cha Uturuki kilikuwa; Demirel, Kaya, Koybasi, Irtegun, Tufan, Kisa, Altintop, Turan, Topal, Bulut na Erdinc.
Brazil: Diego Alves, Danilo, Miranda, Luiz, Luis, Fernandinho, Oscar, Gustavo, Willian, Luiz Adriano na Neymar.
Nahodha wa Brazil, Neymar akisherehekea baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-0 jana dhidi ya wenyeji Uturuki
Neymar (kulia) akijiandaa kumfunga kipa Demirel
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2832023/Turkey-0-4-Brazil-Neymar-scores-twice-Semih-Kaya-goal-Willian-strike-wrap-easy-friendly-win-visitors.html#ixzz3IuZu5r4B
0 comments:
Post a Comment