// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MSUVA ‘AZIMWAGA MATE’ SIMBA NA AZAM - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MSUVA ‘AZIMWAGA MATE’ SIMBA NA AZAM - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Wednesday, November 12, 2014

        MSUVA ‘AZIMWAGA MATE’ SIMBA NA AZAM

        Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
        WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva anazivutia Azam FC na Simba SC, lakini bahati nzuri, au mbaya yuko katika mwaka wa kwanza wa Mkataba wake mpya wa miaka miwili na klabu yake, Yanga SC.
        Simba na Azam FC, zote zilijaribu kutaka kumsajili kijana huyo mwishoni mwa msimu uliopita, lakini zikachelewa na kukuta amekwishasaini Mkataba mpya Jangwani.
        Kwa sasa inaaminika Msuva ndiye winga bora zaidi Tanzania, ingawa ameshindwa kumshawishi kocha wa Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij kumpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.
        Msuva amekuwa mkali kwa misimu takriban miwili akitamba Yanga SC, lakini hata mbele ya kocha aliyetangulia Taifa Stars, Mdenmark, Kim Poulsen hakuwahi kuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza. 
        Tangu ajiunge na Yanga SC akitokea Moro United mwaka 2012, Msuva tayari amekwishaichezea timu hiyo mechi 72 na kuifungia mabao 17.
        Tayari amempiku kwa mbali, mshambuliaji Said Bahanuzi waliyesajiliwa pamoja, akitokea Mtibwa Sugar, ambaye hadi sasa ana mechi 48 na mabao 15, matatu kati ya hayo ya penalti.
        Simon Msuva 'anazitoa udenda' Azam FC na Simba SC

        Bahanuzi alikuwa ana mwanzo mzuri Yanga SC akitoa mchango mkubwa kwa timu hiyo kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame- tena akiibuka mfungaji bora katika michuano hiyo iliyofanyika Dar es Salaam.
        Lakini makali yake yaliyeyuka ndani ya msimu wake huo huo wa kwanza- baada ya kusajiliwa mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbangu, aliyecheza misimu miwili Jangwani.
        Kavumbangu aliondoka Yanga SC mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuichezea timu hiyo jumla ya mechi 63 na kuifungia mabao 31, moja la penalti. Lakini ujio wa Mbrazil Genilson Santana Santos ‘Jaja’ umezidi kumuweka katika wakati mgumu Bahanuzi na tayari kuna dalili za kutosha anaweza kuonyeshwa mlango wa kutokea baada ya msimu huu.
        Said Bahanuzi ameshindwa kabisa kufufua makali yake Yanga SC
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: MSUVA ‘AZIMWAGA MATE’ SIMBA NA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry