// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MSUVA AING'ARISHA YANGA SC TAIFA, APIGA ZOTE MBILI IKIICHAPA MGAMBO 2-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MSUVA AING'ARISHA YANGA SC TAIFA, APIGA ZOTE MBILI IKIICHAPA MGAMBO 2-0 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, November 08, 2014

    MSUVA AING'ARISHA YANGA SC TAIFA, APIGA ZOTE MBILI IKIICHAPA MGAMBO 2-0

    Na Nagma Khalid, DAR ES SALAAM
    MABAO mawili ya Simon Msuva, yameipa Yanga SC ushindi wa 2-0 dhidi ya Mgambo JKT katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Msuva aliyetokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Haruna Niyonzima, alikosekana katika mechi tatu zilizopita kutokana na kuwa majeruhi na leo amerejea na kuwafurahisha wana Yanga.
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Ngole Mwangole wa Mbeya, dakika 45 za kwanza zilimalizika kukiwa hakuna bao. 
    Yanga SC ndiyo waliokuwa wa kwanza kulitia majaribu lango la Mgambo dakika ya nne, baada ya Niyonzima kumpa pasi nzuri Mrisho Ngassa, lakini akazidiwa maarifa na mabeki wa JKT.
    Mgambo walijibu shambulizi hilo dakika moja baadaye, kufuatia Fully Maganga kumtoka vizuri beki Rajab Zahir lakini shuti lake lilidakwa na kipa Deo Munishi ‘Dida’, ambaye hata hivyo aliteleza kabla.
    Mshambuliaji Mbrazil, Genilson Santana Santos ‘Jaja’ aliunganishia juu kidogo ya lango krosi nzuri ya Niyonzima dakika ya 43.
    Kocha Mbrazil wa Yanga SC, Marcio Maximo alianza na mabadiliko kipindi cha pili, akiwaingiza Simon Msuva na Jerry Tegete kwenda kuchukua nafasi za Jaja na Niyonzima.
    Dakika moja tu baada ya kuingia Tegete alikaribia kuifungia Yanga baada ya kuikosakosa kidogo krosi maridadi ya Coutinho ambayo ilikwenda nje.  
    Beki wa Mgambo, Salum Kipaga alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 52 baada ya kumpiga ngumi kwa makusudi Mrisho Ngassa wa Yanga SC.
    Msuva aliifungia Yanga SC bao la kwanza dakika ya 73 baada ya kutumia makosa ya kipa Said Lubawa aliyesita kutokea mpira, akidhani mfungaji huyo ameotea.   
    Msuva tena akawainua vitini mashabiki wa Yanga SC dakika ya 88 akimalizia pasi nzuri ya Hassan Dilunga, akitumia tena makosa ya kipa Lubawa kutoka langoni bila ‘mahesabu’.
    Kwa ushindi huo, Yanga SC inatimiza pointi 13 baada ya kucheza mechi saba na kukabana na Azam FC katika nafasi ya pili kutokana na kulingana pointi.
    Kikosi cha Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Hamisi Kiiza dk65, Rajab Zahir, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Andrey Coutinho, Haruna Niyonzima/Simon Msuva dk46, Genilson Santos ‘Jaja’/Jerry Tegete dk46, Mrisho Ngassa na Hassan Dilunga.
    Mgambo JKT; Said Lubawa, Bashiru Mohamed, Pera Mavuo, Novaty Lufunga, Salum Kipaga, Sabri Makame, Mohammed Samatta/Ramadhani Malima dk59, Ally Iddi, Nassor Gumbo/Hassan Kibakuli dk63, Fully Maganga/Salim Aziz Gilla dk82 na Malimi Busungu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSUVA AING'ARISHA YANGA SC TAIFA, APIGA ZOTE MBILI IKIICHAPA MGAMBO 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top