KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amesema kwamba hajahusika kwa chochote juu ya kuenguliwa kwa Diego Costa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania.
Costa amekuwa akisumbuliwa na maumivu msimu huu, kwanza nyama na sasa kinena.
Amekuwa akitibiwa kwa uangalifu kwenye michezo kadhaa, lakini ataanza leo dhidi ya Liverpool kabla ya kupata mapumziko ya wiki mbili ya kutocheza mechi za ushindani, kufuatia kocha Vicente del Bosque kutomuita kwenye kikosi cha Hispania.
Diego Costa akiwa mazoezini na wachezaji wenzake wa Cheksea huko Cobham mapema wiki hii- ataanza dhidi ya Liverpool leo
Kikois cha Del Bosque kitacheza na Belarus katika mechi ya kufuzu Euro 2016 Novemba 15 kabla ya kuivaa Ujerumani katika mchezo wa kirafiki siku tatu baadaye.
Alipoulizwa kuhusu kutojumuishwa kwa Costa kwenye kikosi cha Hispania, Mourinho alisema: "Nimefurahishwa ndio, lakini nataka kuweka saws hii, sijahusika kwa lolote kwenye uamuzi huo,".
"Hizo siku 15 hatimaye anaweza kupumzika na kufanya kazi vizuri. Ni habari njema kwetu, na nataka kuwashukuru Shirikisho la Soka Hispania kwa uamuzi huo, lakini nataka kuweka sawa sikufanya chochote juu ya yaliyotokea,"amesema.
Mourinho pia amethibitisha mshambuliaji Loic Remy pia atakuwepo kwenye mchezo wa leo baada ya kupona maumivu ya nyonga.
0 comments:
Post a Comment