MBEYA City imechapwa 1-0 na Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kambarage Shinyanga jioni ya leo.
Huo unakuwa mchezo wa tano Mbeya City kufungwa msimu huu, yenyewe ikiwa imeshinda mechi moja na kutoa sare moja- maana yake kocha Juma Mwambusi amekalia kuti kavu.
Timu nyingine ya Mbeya, Prisons imefungwa pia 1-0 na wenyeji Polisi Uwanja wa Jamhiri mjini Morogoro.
Mchezo kati ya wenyeji Mtibwa Sugar na Kagera Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro ulivunjika kutokana na mvua kubwa baada ya kipindi cha kwanza na sasa utamaliziwa kesho.
Mtibwa walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0, lililofungwa na Ame Ally.

0 comments:
Post a Comment