// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MBEYA CITY: DEUS KASEKE NI MALI YETU TU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MBEYA CITY: DEUS KASEKE NI MALI YETU TU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, November 19, 2014

    MBEYA CITY: DEUS KASEKE NI MALI YETU TU

    Na Emanuel Madafa, MBEYA
    KLABU ya timu ya Mbeya City, imesema bado inamshikilia mchezaji wao  Deus Kaseke na kukanusha madai ya kwamba mchezaji huyo anatarajiwa kusajiriwa na timu za Simba na Yanga kupitia dirisha dogo.
    Kiungo huyo mshambuliaji wa kikosi hicho cha Mbeya City, hivi karibuni jina lake limeoneka kuchomoza kwenye vyombo vya habari ikionyesha kwamba mchezaji huyo anakwenda kwa wekundu wa msimbazi Simba sanjari na mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Ame Ali.
    Aidha taarifa hizo zimekuwa zikidai kuwa mchezaji huyo huenda akamwaga wino katika klabu ya Yanga kwa ajili ya kukipiga katika duru la pili.
    Deus Kaseke anatajwa kuwaniwa na vigogo Simba na Yanga, lakini klabu yake Mbeya City imesema hauna taarifa zozote 
    Akizungumza na blog  hii, Katibu mkuu wa klabu hiyo, Emmanuel Kimbe, alisema mpaka sasa uongozi huo haujapata  ofa yoyote kutoka kwenye vilabu hivyo.
    Amesema,  hivyo mchezaji Deus Kaseke anaendelea kuwa mchezaji halali wa klabu ya Mbeya City lakini Kimbe, hakuwa tayari kuweka wazi mkataba walioingia na mchezaji huyo.
    Katibu huyo ameweka wazi kuwa Mpaka sasa bado klabu  hiyo inauhalali wa kuendelea kumtumia mchezaji Deus Kaseke kwani mkataba wake haujamalizika na pia uongozi haujapokea ofa yoyote kutoka klabu za Yanga na Simba.
    Wakati huo huo, timu ya mbeya city inatarajia kuingia kambini mwishoni mwa mwezi huu kujiwinda na duru inayofuata ya ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara.
    Timu hiyo ambayo itafungua dimba na timu ya Ndanda kutokaa Mkoani Mtwara, mchezo unaotaraji kupigwa kwenye dimba la kumbukumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine Jijini Mbeya.
    Hata hivyo, msimu huu timu hiyo haijafanikiwa kufanya vizuri baada ya kufungwa michezo minne kwenda sare michezo mitatu na kupata ushindi wa mchezo mmoja dhidi ya Costunion ya Tanga hivyo kujikusanyia jumla ya pointi 5 ikiwa inaburuza mkia kwenye msimamo wa ligi kuu.
    Mwisho.
    Imehamishwa kutoka http://www.jamiimoja.blogspot.com
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY: DEUS KASEKE NI MALI YETU TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top