Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KOCHA Mkuu wa Yanga SC, Marcio Maximo amesema kwamba ana matumaini ya kushinda mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mgambo JKT Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbrazil huyo, amesema anakiamini kikosi chake kitafanya vizuri katika mchezo na kurudi katika nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Maximo (pichani kushoto) amesema walicheza vizuri mechi tatu zilizopita, wakiambulia pointi nne baada ya sare ya 0-0 na Simba SC, ushindi wa 3-0 na Stand United kabla ya kufungwa 1-0 na Kagera Sugar, matokeo ambayo hakuyategemea.
Lakini amesema anaamini katika Uwanja wa Taifa wana nafasi nzuri ya kupata ushindi na kucheza kandanda safi.
Kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars, amesema wachezaji wote wanatambua umuhimu wa mchezo dhidi ya Mgambo JKT kesho na anawaheshimu wapinzanii wake ni timu nzuri.
Yanga SC iliyoingia kambini jana jioni katika hoteli ya Valley View, Kariakoo, Dar es Salaam, kesho itawakosa Nahodha wake, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu na mshambuliaji Hussein Javu ambaye ni majeruhi.
Yanga SC inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu, nyuma ya Azam FC inayolingana nayo kwa pointi, 10 kila moja, Coastal Union pointi 11 na vinara Mtibwa Sugar pointi 14.

0 comments:
Post a Comment