Na Mwandishi Wetu, CAIRO
KAMPUNI ya Adidas na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) leo Novemba 26, 2014 zimeuwasilisha mpira wa Marhaba, kuwa mpira rasmi wa Fainali za Mataifa Afrika zitakazofanyika Equatorial Guinea mwaka 2015.
Marhaba, utaonyeshwa rasmi Jumatano ya Desemba 3 mwaka 2014 wakati wa droo ya michuano hiyo ukumbi wa Sipopo Convention Centre mjini Malabo.
Teknolojia iliyotumika kutengeneza mpira huo inashabihiana na ile iliyotumika kwenye Brazuca, uliotumika kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil na mpira maarufu daima wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mpira huo wa AFCON ya mwakani utaanza kuuzwa Jumatatu ya Desemba 1, mwaka 2014.

0 comments:
Post a Comment