KLABU ya Manchester United imeichapa mabao 3-0 Hull City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Old Trafford.
Mabao ya United yamefungwa na Chris Smalling dakika ya 16, Wayne Rooney dakika ya 42 na Robin van Persie dakika ya 66.
United ilipata pigo baada ya winga wake, Angel di Maria kutolewa nje dakika ya 14 baada ya kuumia, nafasi yake ikichukuliwa na Ander Herrera.
Katika mechi nyingine, Liverpool imeilaza 1-0 Stoke City bao pekee la Glen Johnson, West Ham imeifunga 1-0 Newcastle bao la Aaron Cresswell, wakati Swansea imetoka 1-1 na Crystal Palace na QPR imeilaza 3-2 Leicester, Burnley ikitoka 1-1 na Aston Villa.
Mchezo uliotangulia jioni ya leo, Arsenal imeichapa 1-0 West Brom bao pekee la Danny Welbeck.
Van Persie wa United akipongezwa na mchezaji mwenake, Rooney baada ya kufunga bao la tatu Uwanja wa Old Trafford
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2854001/Manchester-United-3-0-Hull-City-Robin-van-Persie-goals-Old-Trafford-Louis-van-Gaal-secures-easy-win-Tigers.html#ixzz3KTjD7h8f
0 comments:
Post a Comment