BONDIA Anthony Joshua anayetarajiwa kuwa Lennox Lewis mpya, amempiga mpinzani wake mkongwe Michael Sprott na kuweka rekodi ya kushinda mapambano 10 mfululizo kwa Knockout (KO) tangu aanze ngumi za kulipwa.
Bingwa huyo wa Olimpiki alianza vizuri pambano hilo mjini Liverpool akitamba kuanzia dakika ya kwanza, akimshambulia mfululizo mpinzani wake kiasi cha kumlazimisha refa kuingilia kati kuwaachanisha.
Akiwa na umri wa miaka 39, Sprott alionyesha hizi si zama zake tena za kufurukuta kwenye ndondi za uzito wa juu, akifanya vibaya katika pambano la sita baada ya kupigwa kwa KO Ranudi ya tatu usiku wa jana.
Joshua amefikisha mapambano 10 mfululizo ya kushinda kwa KO
Joshua akishangilia baada ya kummaliza Sprott
0 comments:
Post a Comment