Na Salum Ezry, CAIRO
KOCHA Mkuu wa Misri, Shawky Gharib ameita wachezaji 26 kwa ajili ya mechi mbili zijazo ngumu dhidi ya Senegal na Tunsia kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani, pasipo kumjumuisha kipa mkongwe Essam El Hadary.
Mafarao wana tatizo la majeruhi kwa makipa wake, kutokana na Sherif Ekramy wa Al Ahly kutakiwa kuwa nje kwa miezi miwili na Amir Abdel Hamed naye pia majeruhi. Wote walikuwepo kwenye kikosi cha Mafarao katika mechi zilizopita.
Taarifa nchini Misri zilisema kwamba Gharib angemuita El Hadary kwa ajili ya mechi hizo mbili kutokana na uzoefu wake, lakini kocha huyo amemchukua kipa kinda wa Enppi, Ali Lotfi.
Gharib pia amewatema mchezaji wa Zamalek, Aymen Hefny, beki wa Al Ahly, Saad Samir, Mohamed Abdel-Shafy, mshambuliaji mkali wa mabao wa Al Ahly, Amr Gamal na Nahodha wa Ismailia, Hosny Abd Rabo kutokana na kuwa majeruhi.
Kikosi cha Misri kimesheheni sura mpya kama Arafa Al Sayed, Momen Zakria, Mahmoud Hassan na Mohamed Salem. Mshambuliaji mkongwe wa Al Ahly, Emad Meteb amerejeshwa kwenye kikosi hicho kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya mwaka.
Mabingwa hao wa zamani wa Afrika wataingia kambini mjini Cairo leo.
Kikosi kamili cha Mafarao kinaundwa na makipa; Ahmed El Shenawy (Zamalek), Mohamed Sobhi (Smouha), Ali Lotfi (Enppi), mabeki; Ahmed Elmohamady (Hull City), Hazem Emam (Zamalek), Shawky Al Saied (Ismailia), Ali Gabr (Zamalek), Ahmed Fathy (Umm Selal, Qatar), Sabri Rahil (Al Ahly), Bahaa Magdi (Ismailia) na Salah Soliman (Enppi).
Viungio ni; Amr Al Solyia (Ismailia), Ibrahim Salah (Zamalek), Hossam Ghaly (Al Ahly), Mohamed El Nney (FC Basel), Ibrahim Abdel Khalek (Smouha), Mahmoud Hassan (Al Ahly), Waled Soliman (Al Ahly), Momen Zakaryia (Zamalek) na washambuliaji Ahmed Hamoudi (FC Basel), Mohamed Salah (Chelsea), Emad Meteb (Al Ahly), Arafa Al Sayed (Al Gaish), Khaled Kamar (Zamalek) na Mohamed Salem (Arab Contractors).

Mohamed Salah wa Chelsea ameitwa kikosi cha Misri kuzivaa Senegal na Tunisia |

0 comments:
Post a Comment