Amrouche kushoto akiwa na kocha wa zamani wa Tanzania, Mdenmark Kim Poulsen |
Chanzo cha habari kimesema kwamba mazungumzo baina ya panda hizo mbili yanaendelea vizuri na kwamba Amrouche anaweza kutambulishwa wakati wowote tayari kuanza kazi kwa ajili ya msimu wa 2015 wa KPL.
De Jongh alichukua nafasi ya James Nandwa aliyefukuzwa katikati ya msimu wa 2014 baada ya kuiongoza klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya sita kwenye ligi.
Hata hivyo, kiwango cha timu chini ya kocha huyo Mholanzi hakikuuvutia uongozi wa Leopards na ukawa mwanzo wa kuelekea mlango wa kutokea.
Amrouche alikuwa kocha wa Harambee Stars kuanzia mwaka 2013, lakini akafukuzwa na Shirikisho la Soka Kenya baada ya kushindwa kufuzu kwenye fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2015.
Mshindi wa Kombe la CECAFA Challenge mwaka jana akiwa na Harambee Stars, awali, alifundisha timu za Burundi na Equatorial Guinea.
0 comments:
Post a Comment