Karim Ndungwa ameipigia hat trick Villa jana |
Erisa Ssekisambu aliyetokea benchi alifunga bao la nne akirejea uwanjani kwa mara ya kwanza kufuatia kusimamishwa mwezi mmoja kwa utovu wa nidhamu.
Ndugwa sasa anafikisha mabao saba anayomzidi Robert Ssentongo, na hiyo inakuwa hat-trick ya pili msimu huu.
Matokeo hayo yanaifanya Villa iendelee kuwa nafasi ya pili kwa pointi zake 22, moja nyuma ya vinara, Vipers. Wapinzani wa Villa, Entebbe wanabaki nafasi ya tatu kutoka mkiani kwa pointi zao sita.
Katika mechi nyingine za jana, bao pekee la Joshua Masene liliipa ushindi wa 1-0 Bul dhidi ya waburuza mkia Rwenshama Uwanja wa Kakindu, Jinja wakati Lweza na Bright Stars zilitoka sare ya 1-1 huko Wankulukuku.
Fred Kalanzi aliifungia Lweza wakati Anthony Bongole akawafungia wageni huku Fred Kajoba ikifikisha mechi tatu bila kushinda.
0 comments:
Post a Comment