Na Vincent Malouda, NAIROBI
KOCHA wa timu ya taifa la Uganda, Mserbia Milutin ‘Micho’ Sredojevic amekoseshwa lepe la usingizi kwa taarifa kuwa beki wa kushoto wa Gor Mahia na Mganda, Godfrey ‘Jaja’ Walusimbi hatakuwepo kwenye mechi yao ya raundi ya tano ya kufuzu kushiriki kombe la mabingwa barani Afrika dhidi ya Ghana siku ya Jumamosi tarehe 15 Novemba mjini Kampala, Uganda.
Beki huyo mzoefu anahudumia marufuku ya mechi moja baada ya kulambishwa kadi mbili za manjano kwenye mechi za ugenini dhidi ya Ghana na Togo September 6 na Oktoba 15 mtawalia ndiposa marufuku.
Sijui kwa kweli. Lakini nina uhakika tutafanya vyema sababu ni kazi yetu kujaribu kupata matokeo mazuri wakati mgumu kama huu, Micho aliliambia gazeti la The Observer la nchini Uganda alipoulizwa kuhusu kutokuwepo kwa Walusimbi.
Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa la Rwanda sasa itamlazimu kuwatumia aidha wachezaji Brian Majwega, Alex Kakuba, Fred Nkata, Isaac Muleme au Joseph Ochaya kujaza nafasi hiyo lakini amesistiza kuwa haitakuwa rahisi na itabidi apime uwezo wao wa kujaza pengo hilo kwenye mazoezi kabla ya kudanadana na Black Stars katika uwanja wa Nelson Mandela, Namboole.
Tutaona katika mazoezi lakini kwa sasa siwezi kisia lolote.
Walusimbi hata hivyo anaruhusiwa kucheza mechi yao ya mwisho ya kundi E dhidi ya Guinea iliyoratibiwa kupigwa jumatano tarehe 19 Novemba mjini Casablanca kwa vile atakuwa amemaliza marufuku hayo.
Uganda Cranes wanahitaji matokeo ya kupendaza ili kuweka wazi nafasi yao ya kufuzu fainali za kombe hilo mapema mwaka ujao. Cranes wana pointi nne baada ya mechi nne na wanashikilia nafasi ya tatu kwenye jedwali la timu nne.

![]() |
Kocha wa Uganda, Milutin Sredojevic 'Micho' kushoto |

0 comments:
Post a Comment