Festus Mbewe ameifungia Nkana leo ikiua 6-0 |
TIMU ya Nkana FC imemaliza msimu wa Ligi Kuu ya Zambia 2014 kwa ushindi wa mabao 6-0 leo dhidi ya National Assembly Uwanja wa Woodlands Stadium mjini Lusaka.
Ushindi unakuwa faraja kubwa kwa Nkana iliyoshindwa kutetea ubingwa wa nchi hiyo walioutwaa mwaka 2013, wakimaliza katika nafasi ya nne kwa pointi zao 52, saba nyuma ya Zesco United waliorithi taji hilo.
Mabao ya Nkana yamefungwa na Festus Mbewe, Ronald Kampamba, Derrick Mwansa, Francis Simwanza, Shadrick Musonda na Lottie Nyimbili.
Hata hivyo, Nkana bado ina nafasi ya kutwaa taji mwaka huu, kwani watamenyana na Zesco katika fainali ya Kombe la Barclays Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment