Na Mahmoud ZubeIry, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba milango iko wazi kwa mlinda mlango wao wa zamani, Juma Kaseja kurejea.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Dar es Salaam, kwanza Hans Poppe amesema hawajafanya mawasiliano yoyote na kipa huyo wa Yanga SC, bali wamekuwa wakisoma tu kwenye vyombo vya habari juu ya kurejea kwake, Simba SC.
“Hatujawahi kuzungumza na Kaseja, ila yeye kama anataka kurudi hapa, ni nyumbani. Alikuwepo, akaenda Yanga SC, akarudi na ameenda tena huko, hakuna ubaya akirudi, anakaribishwa tu,”amesema.
Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) amesema hata mara ya mwisho Kaseja hakuondoka vibaya Simba SC, hivyo anakaribishwa wakati wowote.
“Mara ya mwisho aliondoka hapa baada ya Mkataba wake kwisha. Yeye akaona atafute sehemu yenye maslahi zaidi, amekwenda. Ila hapa ni nyumbani kwake, akitaka kurudi wakati wowote milango iko wazi,”ameongeza.
Aidha, Hans Poppe amesema kwamba wanataka kuiandikia barua klabu ya Yanga SC kuto ofa ya kumnunua winga wao, Simon Msuva.
“Labda tu niongeze kwamba, tuna mpango wa kuwaandikia barua Yanga SC, kuwaomba kumnunua Msuva. Ni mchezaji mzuri ambaye tunaona atatufaa katika timu yetu,”amesema.
Hans Poppe alisema yote hayo baada ya kumaliza kumsainisha Mkataba mpya wa miaka miwili, kiungo wa timu hiyo Jonas Mkude, Kawe, Dar es Salaam leo.

![]() |
Hans Poppe kushoto akijadiliana na Rais wa Simba SC, Evans Aveva |

0 comments:
Post a Comment