// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); GOR MAHIA BINGWA KENYA!!! SHEREHE ZANOGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE GOR MAHIA BINGWA KENYA!!! SHEREHE ZANOGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, November 08, 2014

    GOR MAHIA BINGWA KENYA!!! SHEREHE ZANOGA

    Na Vincent Malouda, NAIROBI
    TIMU ya Gor Mahia wamelihifadhi kombe la ligi kuu nchini Kenya baada ya kuwalaza Ushuru FC 3 – 0 kwenye mojawapo ya ngarambe nane zilizokamilisha msimu wa 2014 wa ligi kuu nchini Kenya.
    Kiungo Eric Ochieng’ alifungua nyavu za watoza Ushuru mnamo dakika ya nane ya muda wa maongezi kipindi cha kwanza baada ya mabeki wa Ushuru kusinzia kabla ya mzawa wa Uganda Dan Sserunkuma kucheka na nyavu bao la pili dakika ya 51.
    Sserunkuma aliifikia krosi ya George ‘Blackberry’ Odhiambo kwenye shambilio shutukizi kabla ya kuelekeza ngoma hiyo pembeni mwa nyavu za mlindamlango wa Ushuru Kevin Otieno.

    Ni bao lake Richard Mmboyi hata hivyo lililowazuzua halaiki ya mashabiki wa K’Ogalo kwa kupiga ngoma, vifijo na nderemo uwanjani kwani beki huyo wa kushoto wa Ushuru alifunga bao la tatu kwenye neti yake dakika ya 78 alipojaribu kuzima shuti la Godfrey Walusimbi.
    Vijana hao wa Msikochi Frank Nuttal sasa wamefikisha mataji kumi na manne ya ligi kuu, mawili zaidi ya wapinzani wao AFC Leopards ambao waliwaramba Bandari 3 – 2 katika uga wa Kaunti ya Mombasa. Gor sasa wanamaliza msimu kwa alama 60, alama tatu mbele ya nambari mbili Sofapaka aliyetoka sare ya kufungana mabao mawili kwa mawili na Tusker FC ugani Ruaraka. Pia, wanakwenda nyumabni na kitita cha milioni nne shilingi za Kenya.
    Kwenye mtanange huo, vijana wa Sam Timbe Sofapaka walitoka nyuma ya goli moja na kutoka kufanya mambo kuishia 2 - 2. Kiungo Brian Osumba alifunga bao la kwanza la Wanamvinyo dakika ya 42 kabla ya raia wa Burundi Fiston Aboul kuzawazisha dakika ya 53 kisha Antony Ndolo akawapa Batoto ba Mungu bao la pili dakika ya 84 lakini Jesse Were akafunga penalti dakika za lala salama na kuhakikisha wanahifadhi rekodi yao ya kulazwa mechi moja tu nyumbani msimu huu chini ya ukufunzi wake aliyekuwa kocah wa timu ya taifa Harambee Stars Francis Kimanzi.
    Kwenye mechi zingine, Nairobi City Stars walishushwa daraja rasmi baada ya kutoka sare tasa na Mathare United kwenye uchanjaa wa Hope Centre huku wenzao watakaojiunga nao kwenye daraja la pili Top Fry AllStars pia wakigaragazwa magoli 3 – 2, Thika United 0 – 0 Chemelil Sugar uwanjani Thika, SoNy Sugar 1 – 0 Ulinzi Stars, Western Stima 0 – 2 Muhoroni Youth.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GOR MAHIA BINGWA KENYA!!! SHEREHE ZANOGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top