Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KIUNGO mkabaji wa zamani wa Uganda, The Cranes- George ‘Best’ Nsimbe amewasili leo Dar es Salaam, tayari kusaini Mkataba wa kuwa kocha wa Azam FC Jumatatu, imeelezwa.
Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa ‘Father’ ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Nsimbe aliyekuwa akiifundisha KCCA ya Uganda, atakuwa Msaidizi wa Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mcameroon, Joseph Marius Omog.
Nassor amesema hiyo inafuatia kwa aliyekuwa koha Msaidizi kwa miaka minne iliyopita, Muingereza Kali Ongala kujiuzulu wiki iliyopita na klabu imeamua kumuita Nsimbe baada ya kuvutiwa na mafanikio yake KCCA.
George Best' Msimbe ametua kupiga kazi Azam FC |
Nsimbe atakuwepo leo jukwaani Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuishuhudia timu hiyo ikimenyana na Coastal Union Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Azam FC, inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kujiweka sawa katika harakati za kutetea ubingwa wake, baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo, 1-0 na JKT Ruvu na 1-0 na Ndanda FC.
Azam ina pointi 10 sasa katika nafasi ya tatu, sawa na Yanga SC iliyo nafasi ya nne- wote wakiwa nyuma ya Coastal pointi 11 na Mtibwa Sugar pointi 14 kileleni.
0 comments:
Post a Comment