MSHAMBULIAJI Radamel Falcao yuko tayari kuongeza nguvu kikosini Manchester United katika mechi dhidi ya Hull City Uwanja wa Old Trafford Jumamosi baada ya kupona maumivu yake.
Nyota huyo wa Colombia amekuwa akisumbuliwa na maumivu tangu amejiunga na United kwa mkopo kutoka Monaco msimu huu na hajacheza kwa wiki tano sasa.
Lakini kocha Louis van Gaal amesema Falcao anajiandaa kurudi kikosini mwishoni mwa wiki hii, na Marcos Rojo anaweza pia kuorodheshwa baada ya kupona maumivu ya bega aliyopata katika mechi ya mahasimu wa Jiji la Manchester mwanzoni mwa mwezi huu.
Manchester United wametweet picha hii ya Falcao kurejea mazoezini wiki hii
Manchester United inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England kuelekea mechi ya mwishoni mwa wiki
0 comments:
Post a Comment