![]() |
Didier Zakora amekataa wito Ivory Coast |
Zokora, mwenye umri wa miaka 33, ambaye kwa sasa anachezea Akhisar Belediyespor ya Uturuki, alistaafu soka ya kimataifa Julai mwaka huu kufuatia Tembo wa Ivory Coast kufanya vibaya katika Fainali za Kombe la Dunia 2014.
Pamoja na hayo, kocha wa Ivory Coast, Herve Renard amemuita tena kikosini na beki wa Liverpool, Kolo Toure baada ya timu hiyo kuruhusu mabao tisa katika mechi tatu zilizopita za kufuzu AFCON, hali ambayo wachambuzi wengi wamesema imetokana na ubutu wa safu ya ulinzi.
“Ni masikitiko makubwa, naandika juu ya wito wangu kwenye timu ya taifa ya Ivory Coast kwa mechi zijazo za kufuzu. Sitajuwepo kwenye kikosi cha Tembo,” amesema Zokora katika taarifa yake kwa Shirikisho la Soka Ivory Coast.
“Nimeitumikia nchi yangu kwa furaha, lakini nafikiri ukurasa umegeuka,” amesema. Ivory Coast itacheza na Sierra Leone Novemba 14 na Cameroon Novemba 19, mechi zote zikipigwa mjini Abidjan.
Wakiwa wanashika nafasi ya tatu katika Kundi D kwa pointi zao sita nyuma ya Cameroon wenye 10 na DRC sita, Ivory Coast wanatakiwa kushinda mechi zote ili kuangalia uwezekano wa kufuzu.
0 comments:
Post a Comment