BONDIA Chris Eubank Jnr ndiye mwanandondi mwenye kipaji zaidi tangu zama za Sugar Ray Leonard na mwanamasumbwi hatari zaidi duniani, amesema baba yake.
Eubank Jnr, mwenye umri wa miaka 25, hajapoteza pambano hata moja licha ya kupigana mara 18 hadi sasa katika ngumi za kulipwa, lakini anakabiliwa na mtihani wa kulinda rekodi yake atakapopigana na Billy Joe Saunders kuwania mataji ya Uingereza, Ulaya na Jumuiya ya Madola uziti wa Middle ukumbi wa ExCeL Arena mjini London Jumamosi.
Chris Eubank Snr, bingwa wa dunia wa uzito wa aina mbili tofauti na mmoja wa mabondia wakali kuwahia kutokea Uingereza, pia amesema hata yeye hafikii makali ya mwanawe huyo.
Chris Eubank Jnr (kushoto) ndiye bondia mwenye kipaji na hatari zaidi duniani kwa sasa kwa mujibu wa baba yake
Chris Eubank Jnr akipigana mazoezini kujiandaa na pambano dhidi ya Billy Joe Saunders Jumamosi
"Mwanangu ndiye mtu hatari zaidi ambaye sijawahi kukutana naye katika ngumi, mpiganaji hatari zaidi ulimwengu,".
Leonard anasifika kama mmoja wa mabondia wakubwa kuwahi kutokea duniani, na bora zaidi zaidi ya wengi waliowahi kutokea.
Mmarekani huyo alishinda Medali ya Dhahabu ya Olimpiki mjini Montreal mwaka 1976 kabla ya kishinda mataji ya dunia ya ngumi za kulipwa katika madaraja matano ya uzito tofauti.
Mapambano yake dhidi ya Roberto Duran, Thomas Hearns na Marvin Hagler yatabakia kuwa ya kukumbukwa zaidi katika historia yake ya uligoni.
0 comments:
Post a Comment