KOCHA Brendan Rodgers amekiri kwamba amekalia kuti kavu baada ya Liverpool kuchapwa mabao 3-1 na Crystal Palace jana na sasa anapambana kuokoa kibarua chake.
Rodgers amesema alikuwa na mazungumzo na wamiliki wa Liverpool ambao ni Wamarekani juu ya mwenendo mbovu wa timu hiyo, ambao unawafanya wazidiwe pointi 18 na vinara Ligi Kuu ya England, Chelsea.
Brendan Rodgers yuko katika wakati mgumu Liverpool akiwa ameshinda mechi mbili tu katika Ligi tangu Agosti
"Kocha yeyote atakuambia kwamba unapaswa kushinda na kupata matokeo, hususan kwa namna ambavyo tumeiendeleza klabu,"amesema. Rodgers, ambaye baadaye alidokeza katika chumba cha kubadilishia nguo kwamba: "Mimi si kiburi kiasi cha kutosha kufikiri niko salama kwa kila kitu. Nina mawasiliano makubwa na wamiliki. Tumepeana ukweli wa kutosha kila mmoja kwamba tunatakiwa kuoata matokeo. Unatakiwa kucheza, wamiliki na Wakurugenzi na Mwenyekiti wanataka kuona maendeleo uwanjani,".
0 comments:
Post a Comment