Na Abdul Salim, DAR ES SALAAM
MKATABA wa Katibu wa Yanga SC, Benno Njovu unamalizika leo na kwa bahati mbaya klabu hiyo haina mpango naye tena.
Habari kutoka ndani ya klabu hiyo, zimesema kwamba Njovu ni mtu safi, lakini uongozi umebaini masuala ya soka ‘yanampiga chenga’ kidogo, hivyo wanahitaji mtu mwingine katika nafasi hiyo.
Habari zaidi zinasema kwamba, tayari Njovu amekwishafungasha kila kilicho chake kutoka katika ofisi aliyorithi kwa Lawrence Mwalusako, beki wa zamani wa Yanga SC.
Benno Njovu amemaliza Mkataba Yanga SC na klabu hiyo haina haja naye tena |
Bado haijulikani nani atarithi nafasi ya Njovu, lakini BIN ZUBEIRY inafahamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji atafanya mabadiliko zaidi katika Sekretarieti ili kutafuta ufanisi.
0 comments:
Post a Comment