KAMA ingekuwa sinema ya Hollywood, ingekuwa bomba sana.
Lakini Mickey Rourke hakuwa anaigiza jana wakati alipopanda ulingoni baada ya miaka 20 ya kuachana na ndiondi na kumpa mtu kichapo.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 62 alizipiga na Elliot Seymour, mwenye umri wa miaka 33, katika pambano la raundi tano Moscow, Urusi. Rourke alihitaji randi mbili tu kumsimamisha mpinzani wake ambaye alianguka chini baada ya kupewa 'mkono mkali' wa mtu mzima huyo.
Baada ya mapambano 30 katika ngumi za Ridhaa, miaka ya 1960 hadi 70, ambayo alipoteza matatu tu, Rourke alihamia kwenye kucheza filamu Hollywood, kabla ya kurejea kwenye mchezo kama bondia wa kulipwa miaka ya 90, ambayo ilimsababisha athari usoni mwake na kulazimika kufanyiwa upasuaji uliobadilisha mwonekano wa sura yake. Alishinda pambano moja tu kati ya tisa ya kulipwa.
Nyota wa Hollywood, Mickey Rourke akiinuliwa mkono kutangazwa mshindi baada ya kumkalisha Elliot Seymour raundi ya pili
0 comments:
Post a Comment