BONDIA mkongwe Bernard Hopkins atarejea ulingoni licha ya kipigo cha mwishoni mwa wiki kutoka kwa Mrusi, Sergey Kovalev, amesema babe huyo mwenye umri wa miaka 49 jana.
Hopkins, ambaye alishindwa kushinda hata raundi moja katika pointi za majaji wote matatu kwenye pambano hilo la uzito wa Light-Heavy la kuunganisha mataji, amezima tetesi za kustaafu kwake kwa kusema atapigana 'mara moja zaidi.'
"Nani nitapigana naye? Sijui,"amesema Hopkins katika mahojiano ya simu kutoka nyumbani kwake, Delaware. "Lakini atakuwa mtu fulani ambaye ni mkali, na ninataka kupigana na mkali,".
Bingwa wa zamani wa dunia, Bernard Hopkins amesema atapigana 'mara moja zaidi' kabla ya kustaafu
Sergey Kovalev akimpeleka chini Hopkins katika raundi ya kwanza, ingawa alifanikiwa kumaliza raundi 12
Hopkins akiwa ameanguka chini baada ya konde la mpinzani wake
Hopkins, aliyefanikiwa kutetea vizuri kwa rekodi ubingwa wa uzito wa Middle mara 20 kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 na hajawahi kuangushwa chini kabla, lakini aliangushwa kwa mara ya kwanza Jumamosi katika raundi ya kwanza na Kovalev.
Pamoja na hayo alisimama na kuendelea na pambano hadi kupoteza kwa pointi dhidi ya kijana huyo aliyemzidi umri wa miaka 18.
Na huwezi kuamini, bondia huyo anayejulikana kwa nina la utani kama The Executioner alirudi mazodzi tena gym Jumatatu, yaani wastani wa siku moja baada ya pambano lake.
0 comments:
Post a Comment