Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
AZAM FC imewasilisha barua rasmi Simba SC ya kumuomba kiungo Amri Ramadhani Kiemba, ambaye kwa sasa yupo kwenye matatizo na klabu yake.
Rais wa Simba SC, Evans Eliza Aveva ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Azam wametuma barua kumuomba mchezaji huyo ambaye Mkataba wake unaisha Juni mwakani.
“Tumepokea barua ya Azam FC kumtaka Kiemba, baada ya hapo nitaitisha Kikao cha Kamati ya Utendaji kujadili ombi lao, kisha tutawapa majibu,”amesema Aveva.
Mwishoni mwa mwezi uliopita, Kiemba pamoja na viungo wengine wa klabu hiyo, Shaaban Kisiga ‘Malone’ na Haroun Chanongo walisimamishwa Simba SC kwa sababu tofauti.
Wakati Kiemba na Chanongo walidaiwa kucheza chini ya kiwango chao tofauti na wanavyokuwa timu ya taifa, Taifa Stars- Kisiga alidaiwa kuwatolea majibu ya kifedhuli viongozi.
Wachezaji hao walipatwa na mkasa huo baada ya timu kulazimishwa sare ya tano mfululizo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, 1-1 na Prisons mjini Mbeya.
Baada ya kusimamishwa kwao, Simba SC ilitoa sare tena na Mtibwa Sugar mjini Morogoro kabla ya kushinda mechi ya kwanza mwishoni mwa wiki dhidi ya Ruvu Shooting 1-0 mjini Dar es Salaam.
Wachezaji wote baada ya kusimamishwa walitakiwa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Nidhamu ya klabu hiyo, lakini hawakutokea na wakati bado uongozi wa Simba SC haujatangaza hatua zaidi, Kiemba anapata ofa ya kwenda Azam FC.

![]() |
Amri Kiemba anatakiwa Azam FC |

Rais wa Simba SC, Evans Aveva (katikati). Kulia kiungo Jonas Mkude na kushoto Zacharia Hans Poppe, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili |
0 comments:
Post a Comment