// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AVEVA ASEMA; “SIMBA SC HATUNA NAFASI YA KUSAJILI MSHAMBULIAJI WA KIGENI, IZUCHUKWU ATATUSAMEHE” - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AVEVA ASEMA; “SIMBA SC HATUNA NAFASI YA KUSAJILI MSHAMBULIAJI WA KIGENI, IZUCHUKWU ATATUSAMEHE” - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, November 19, 2014

    AVEVA ASEMA; “SIMBA SC HATUNA NAFASI YA KUSAJILI MSHAMBULIAJI WA KIGENI, IZUCHUKWU ATATUSAMEHE”

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    RAIS wa Simba SC, Evans Elieza Aveva amesema kwamba hawana nafasi ya kusajili ya mshambuliaji wa kigeni na kwamba Emmanuel Okwi, Amisi Tambwe na Paul Kiongera wanawatosha.
    Kauli hiyo ya Aveva inakuja wakati tayari vyombo vya habari vimekuwa vikiwahusisha washambuliaji Mnigeria, Emeh Izuchukwu na Mganda Danny Sserunkuma kusajiliwa na Wekundu hao wa Msimbazi.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, Aveva amesema kwamba Izuchukwu ambaye ni mchezaji wao wa zamani, ameomba mwenyewe kurejea kuchezea klabu hiyo, lakini anasikitika hawana nafasi ya mchezaji wa kigeni.
    Rais wa Simba SC, Evans Aveva (katikati) amesema hawana nafasi za kusajili mshambuliaji wa kigeni

    “Hao wachezaji wengine hao, ni magazeti tu yamekuwa yakiandika, lakini ukweli ni kwamba hatujazungumza nao,”amesema Aveva.
    Mbali na Mganda, Okwi, Mrundi Tambwe na Mkenya Kiongera, wachezaji wengine wa kigeni Simba SC ni beki Mganda, Joseph Owino na kiungo Mrundi Pierre Kwizera na kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu, ili klabu isajili mgeni mwingine, italazimika kupunguza mmoja.
    Wakati huo huo: Kocha Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Matola amesema kwamba kikosi cha klabu hiyo kinatarajiwa kuanza mazoezi Jumatatu kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakayorejea mwishoni mwa mwezi ujao baada ya kusimama tangu wiki iliyopita.
    Wachezaji wa kigeni wa Simba SC waliopewa mapumziko ya wiki moja sawa na wazawa, wanatarajiwa kuanza kuwasili Dar es Salaam kuanzia mwishoni mwa wiki hii tayari kuanza mazoezi Jumatatu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AVEVA ASEMA; “SIMBA SC HATUNA NAFASI YA KUSAJILI MSHAMBULIAJI WA KIGENI, IZUCHUKWU ATATUSAMEHE” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top