WASHIKA Bunduki, Arsenal wamefuzu kuingia hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund Uwanja wa Emirates katika mchezo wa Kundi.
Yaya Sanogo aliifngia Arsenal bao lake la kwanza kwenye mechi ya mashindano dakika ya pili, ingawa kinda huyo Mfaransa alionekana kama alikuwa ameotea.
Alexis Sanchez akaifungia timu ya Arsene Wenger bao la pili dakika ya 57 na kuihakikishia kuingia hatua hiyo ya mtoano.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Martinez, Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Arteta/Flamini dk66, Oxlade-Chamberlain/Campbell dk89, Ramsey, Cazorla, Sanchez, Sanogo/Podolski dk78.
Borussia Dortmund; Weidenfeller, Piszczek, Subotic, Ginter, Schmelzer, Gundogan, Bender, Grosskreutz, Immobile/Kagawa dk60, Mkhitaryan na Aubameyang/Ramos dk60.
Alexis Sanchez akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la pili dhidi ya Borussia Dortmund
Sanogo akifumua shuti kumtungua kipa wa Dortmund, Weidenfeller (kulia) kuifungia Arsenal bao la kwanza
PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-2850813/Arsenal-2-0-Borussia-Dortmund-Yaya-Sanogo-Alexis-Sanchez-strike-secure-16-spot-Arsene-Wenger-s-side.html#ixzz3KDZpStfW
0 comments:
Post a Comment